Karibu Sana!

FLAMINGO GARDEN INN, Dar es salaam Tanzania ni mgahawa unaotoa huduma ya vyakula vya asili ya Kitanzania. Nyama choma ya mbuzi, ng’ombe, kuku wa kienyeji na kisasa pamoja na samaki aina ya changu, kolekole, pelege, Jodari, sato na sangara, vyote vinapatikana. Vyakula hivi vinaliwa kwa wali, ugali, pilau, viazi, chips na mbogamboga kama vile mchicha, kisamvu, matembele, mlenda na njegere. Michemsho na makange ya kila aina vipo.

Asubuhi kifungua kinywa, kuna supu ya asili kwa mfano, mtori na vitafunwa kama vile chapati, sambusa, maandazi na vitumbua pamoja na chai tamu ya maziwa yenye viungo vya kiasili.
Mapishi yanaendana na matakwa ya mteja na tunatumia viungo tofautitofauti.

Tuna ukumbi wa sherehe na mikutano wenye nafasi zisizopungua 60. Huduma ya chakula inatolewa kulingana na matakwa ya mteja.
FLAMINGO GARDEN INN imejengwa kiutamaduni. Paa la makuti, ukumbi na usanifu wa jengo kwa ujumla wake ni sanaa halisi ya Kiafrika.
Kuna nafasi tele za kujipumzisha chini ya kivuli cha miti ndani ya bustani ya kitropiki iliyonakishiwa na ndege wa Flamingo wakielea kwenye bwawa la maji.
Kwa ujumla, Flamingo Garden Inn ni kivutio cha kipekee.

FLAMINGO GARDEN INN iko Kinyerezi, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam umbali wa dakika 15 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Karibu sana!

Timu ya FLAMINGO GARDEN INN